Chama
 cha Wananchi (CUF), kimetakiwa kuacha kufuatilia na kuhoji uhalali wa 
kikao cha Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Mapinduzi( CCM) kufanya vikao 
vyake Ikulu kwa madai kuwa kufanya hivyo ni kutumia rasilimali za umma 
kwa maslahi ya chama.
Aidha
 taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu  wa Umoja wa Vijana wa CCM 
(UVCCM), Shaka Hamdu Shaka ,kwa vyombo vya habari  jijini Dar es salaam,
 imesema hoja hiyo iliyotolewa na kiongozi wa CUF, Mbarara Maharagande 
kushutumu hatua hiyo haina mashiko.
“UVCCM
 tunamwambia mwanasiasa huyo, amekwenda kombo, hajui kulinganisha wala 
kutofautisha mambo, alichokisema ni porojo tu na hiyo taarifa 
aliyoiandika kwa umma haina mantiki, haikuwa na kichwa wala 
miguu,kiufupi haikueleweka na kufahamika alichokusudia kukisema”amesema Shaka.
Shaka
 amesema kuwa Viongozi mbalimbali wa Upinzani wamekuwa wakialikwa Ikulu 
na kutumia rasilimia hizo ikiwemo kuandaliwa chakula na vinywaji.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon