Namna Rahisi ya kumjua Mchawi Unapoishi

ukitaka kumjua mchawi mahali unapoishi au unapofanyia kazi, mara nyingi anakuwa na tabia isiyofanana na wengine. Mfano, asubuhi ukiamka, ukiwa unakwenda chooni, ukikutana na jirani yako ukamsalimia lakini akaitikia kwa sauti ya chini sana tena huku akiangalia ukutani, tambua huyo ni mchawi.
Au, unakwenda kazini, kufika unakutana na mfanyakazi mwenzako, unamsalimia kwa kumpa mkono yeye anaitikia salamu lakini hakupi mkono tambua huyo ni mchawi. hakuna mchawi asiyekuwa na dalili kwenye jamii, sema tu macho ya watu yamefungwa kuona yaliyo sirini kutokana na wingi wa dhambi zetu sisi wanadamu.
Mitaani tunapotembea, kuna viumbe vingi sana tunapishana navyo, vinatuona lakini sisi hatuvioni. Mbaya zaidi, viumbe hivi wakati mwingine vinaingia kulala kwenye majumba yetu baada ya kuchoka kwa shughuli zao za mchana kutwa.
Sema usiri wake ni kwamba, baadhi ya viumbe havina ubaya na binadamu, hata vikiingia ndani kwako vinataka hifadhi ya malazi tu asubuhi zinaondoka.
Umewahi kuwa peke yako usiku chumbani halafu ukajisikia hali ya kuogopa sana kiasi kwamba hutaki hata kulala na giza, unawasha taa mpaka kuna kucha? Basi tambua kwamba, kuna viumbe visivyoonekana vimeingia kulala chumbani kwako. Unaposhtuka na kuangalia dirishani vyenyewe vinakuona na kukucheka.
Kifupi kila unachofanya vinaona ila havina dhamira ya kukuzuru.
Sasa utajuaje kuwa ulilala na viumbe? Mara nyingi hivi viumbe humsababishia hali ya kwenda chooni mtu kila wakati. Unaweza kutoka chooni usiku mara nne, wakati si kawaida yako, jua ulilala na viumbe.
Kikubwa, kama unahisi hatari hiyo, ukilala usifunge mlango, yaani ukae wazi. Viumbe hawa huwa hawana ubavu wa kuingia kwenye chumba au nyumba yenye mlango wazi.
Umewahi kutembea usiku peke yako ukafika mahali kwa mbele kama kuna watu au mtu lakini ukifika hakuna? Jua maeneo hayo kuna viumbe visivyoonekana. Na mara nyingi ukikutana na hali hii lazima itaambatana na hisia za nywele kusisimka kichwa kizima.
unaweza ukahisi nywele zinanyonyoka kwa jinsi zinavyosisimka, ujue ni maeneo yenye viumbe.
Tabia ya viumbe hivi ambavyo asili yake ni kutoka Nchi ya Wachawi, ni kupenda maeneo yenye watu wengi, mfano, sokoni, stendi ya mabasi na vituo vya daladala. Hakuna maeneo Dar es Salaam yana viumbe wa ajabu kwa wingi kama stendi ya mabasi, pale Ubungo na katikati ya mitaa ya Kariakoo.
Kwa Ubungo, unapoona watu wengi wakiingia na kutoka huku wamebeba mizigo, nyuma yao kuna viumbe hao, ndiyo maana huwa tunasema watu wengi, lakini ukweli ni kwamba tunawachanganya na viumbe.
Sasa ubaya wao hawa viumbe ni pale wanapoamua wakati mwingine kujitokeza na kuwa watu wanaoweza kuonekana kwa macho.
Hapo ndipo wanapoweza kuharibu eneo. Mfano, usidhani kilio cha mara kwa mara cha foleni jijini Dar es Salaam ni cha kweli, foleni nyingine tunaongezewa na hawa viumbe baada ya kujigeuza na kuwa binadamu.
Wana uwezo wa kufanya magari yao, wakatoka Kariakoo kwenda Kimara, kwenda Mwenge au Kibamba na wanapokuwa Magomeni na wao wanakuwa kwenye foleni wakati wana uwezo wa kufika wanakokwenda bila kuwepo kwenye foleni wala kuwa kwenye magari.
Tatizo ni kwamba, hata ukiliona gari la kiumbe kisichoonekana huwezi kulijua, lina namba za kawaida, kila kitu cha kawaida.
Ila, mara zote abiria wa magari haya hawazidi watatu ikiwa na pamoja na dereva. Na mara zote ndani ya gari kunakuwa na utulivu, hakuna anayeongea wala kucheka, mwanzo wa safari yao hadi mwisho.
Hatari iliyopo ni kwa wale wafanyabiashara wanaouza maji, juisi, sabuni au bidhaa nyingine kwa wenye magari.
Naamini hapa nimeeleweka, yaani ni kwamba, ukifika Magomeni Mapipa, si kuna foleni halafu kuna vijana wanauza vitu kwa watu waliomo ndani ya magari? Basi wale vijana wako hatarini zaidi.
Kwanini? Kwa sababu baadhi ya watu wanaowauzia ni wale viumbe wasioonekana ambao siku hiyo wanakuwa ndani ya gari.
Wana tabia ya kuchukua damu ya vijana kama hao na kwenda kuichafua, baada ya muda utakuta kijana anakuwa mdhaifu, hana maendeleo, mwili unakuwa umechoka, yaani anakuwa binadamu ilimradi anaishi lakini kwa upande mwingine si binadamu kamili.
 
Previous
Next Post »

COMMUNITY HELP