Serikali
 ya China imetoa ufadhili wa ujenzi wa uwanja wa Michezo kwa shule ya 
msingi Msoga iliyopo halmashauri ya wilaya ya Chalinze….
Akizungumza
 katika hafla ya kuoneshwa eneo patakapojengwa uwanja huo  Rais mstaafu 
wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete  ameishukuru serikali ya China kwa 
msaada huo kwakuwa Michezo ni Kitu muhimu kwa watoto huku akitoa rai kwa
 halmashauri ya chalinze kulinda eneo hilo. 
Kwaupande
 wake mwakilishi wa balozi wa China amesema kuwa China inajivunia 
uhusiano mwema uliopo kati ya China na Tanzania,na watahakikisha 
wanajenga uwanja huo kwa wakati ili kuwapa fursa watoto kufurahia 
michezo.
Nae
 Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ametoa rai kwa wananchi wake 
kuhakikisha eneo lililotengwa linalindwa ili dhamira ya china kujenga 
uwanja huo itimie
Ufadhili
 wa ujenzi wa uwanja huo wa michezo kwa watoto wa Msoga ni muendelezo wa
 ufadhili wa China katika kijiji cha Msoga baada ya kujenga shule ya 
msingi Msoga.
Sign up here with your email



ConversionConversion EmoticonEmoticon