Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji
MWANAFUNZI wa mwaka wa kwanza aliyekuwa anachukua shahada ya
ualimu Chuo cha Ajuco (zamani Chuo cha Mtakatifu Agustino, tawi la
Songea) mkoani Ruvuma, Henri Mwilang’ombe (24) amejinyonga kwa kutumia
nguo yake.
Henri alikutwa amejinyonga kwenye kichaka majira ya mchana jana jirani
na shule ya sekondari ya wasichana Songea (Songea Girls) na katika mfuko
wa suruali aliyovaa ameacha ujumbe unaosema; “Nimeamua kujinyonga ili
nisiendelee na mateso ninayopata kutokana na ulemavu wa mguu ambao
wanafunzi wenzangu wananicheka”.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji alithibitisha kutokea tukio hilo.
Kamanda alisema mwanafunzi huyo amefahamika kuwa ni mwanafunzi wa chuo
hicho kutokana na simu zake mbili alizokutwa nazo aina ya Nokia na baada
ya Polisi kupiga baadhi ya namba watu waliopigiwa walisema ni
mwanafunzi wa Ajuco.
Hata hivyo, alisema bado Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kuhusu
tukio hilo ambapo mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha
kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon