Mzee wa Upako adai kuneemeka kwa mgogoro

Dar es Salaam. Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo amesema changamoto alizokutana nazo kwenye nafasi yake ya utumishi zimekuwa chanzo cha kupata zawadi ya magari mawili mapya likiwamo aina ya Toyota Land Cruiser lenye thamani ya Sh200 milioni.

Mchungaji huyo maarufu kwa jina la Mzee wa Upako ametoa kauli hiyo mbele ya waumini wake jana katika kanisa hilo lililopo Ubungo, Kibangu jijini hapa ikiwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya kila Jumapili.

Katika mahubiri hayo, Mzee wa Upako pia amekuwa akijibu mapigo baada ya kuzagaa kwa taarifa iliyoambatana na video iliyomuonyesha akijibizana na jirani yake, huku akimtishia kifo.

Pia, wiki iliyopita alitoa utabiri kwamba waandishi wa habari walioandika habari za kumchafua watakufa kabla ya Machi 2017, vinginevyo ataacha kuhubiri na kwenda kuuza gongo.
Previous
Next Post »

COMMUNITY HELP