
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema wananchi kutumia mabango kueleza
kero zao ni ushahidi kwamba watendaji na madiwani hawawapi nafasi ya
kueleza shida zao.
Majaliwa amesema kwa kutambua hawana nafasi ya kuuliza maswali, wananchi
walitumia mabango katika kila mkutano aliohutubia ili kutoa waliyonayo
moyoni.
Akizungumza katika mkutano wa kuhitimisha ziara yake mkoani Arusha,
Waziri Mkuu alisema ni wazi kuwa viongozi wa serikali ngazi ya wilaya,
kata na vijiji hawaandai mikutano na kuzungumza nao.
“Endapo mngekuwa mnaandaa mikutano ya hadhara, wananchi wasingeomba
kujua lini watapata kiwanja cha kujenga kanisa lao mbele ya Waziri
Mkuu,” alisema.
Kwa habari zaidi nunua nakala yako ya NIPASHE LEO
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon