
Kukua kwa teknolojia ya simu za Smartphone kumekuja na changamoto kubwa kwa baadhi ya makampuni yanayotengeneza simu za mkononi. Kampuni ya Blackberry ni moja kati ya makampuni yaliyokiri kupata hasara kubwa baada ya kushindwa kwenda sawa na mahitaji ya wateja wake.

Blackberry imekiri
kupoteza kiasi cha dola za Marekani milioni 372 baada ya simu yake mpya
aina Q2 kutofanya vizuri baada ya kuingizwa sokoni, Hasara hiyo
imepelekea kampuni ya Blackberry kutangaza kuacha kutengeneza simu za
Smartphone.
Ikumbukwe
kuwa BlackBerry ndio kampuni ya kwanza duniani kutengeneza simu za
Smart, kutoka nchini Canada, ambao wametangaza maamuzi hayo jana
September 28, 2016, na kuliacha jukumu hilo kwa kampuni rafiki ya PT Tiphone Mobile Indonesia Tbk kutoka Indonesia, ambapo wao wataendelea na kazi ya kubuni software na huduma muhimu za simu hiyo.

Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon