Wananchi wa kijiji cha Kingole wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma wamesema
kwa Zaidi ya miaka arobaini toka kuanzishwa kwa kijiji hicho hawakuwahi
kupata barabara hali iliyowalazimu wagonjwa wakiwemo akina mama
wajawazito kutembea kwa miguu takriban kilomita 30 kufuata huduma za
matibabu.
Kero ya ukosefu wa barabara imeghalimu maisha ya wananchi wengi ambao
wamepoteza maisha kwa kufia njiani kwa sababu ya kuchelewa kupata
matibabu.
Wananchi hao wamesema baada ya kufikisha kilio chao kwa viongozi wenye
dhamana ya kulinda maisha yao miaka mitatu iliyopita wakala wa barabara
TANRODS mkoa wa Ruvuma wamejenga barabara kutoka Peramiho hadi Kingole
kwa kiwango cha changalawe kupitia channel ten wameishukuru serikali ya
mkoa wa Ruvuma kwa kusikia kilio chao.
Mhandisi wa TANRODS mkoa wa Ruvuma Lazeck Alinanuswe amekili kuwa
barabara ya Kingole haikuwahi kujengwa lakini sasa wananchi hao
watasahau shida zao baada ya serikali kutoa fedha za ujenzi wa barabara
ya kilomita 80.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt.Binirithi Saatano Mahenge ametembelea barabra
hiyo kutoka Peramiho hadi Kingole ili kujiridhisha kama imejengwa kwa
kiwango kinachotakiwa kabla ya mvua haijanyesha.
Mkoa wa Ruvuma una wilaya sita Halmashauri saba na vijiji Zaidi ya 540 Geofrey Nilahi Channel ten Songea.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon