Mwalimu wa shule ya msingi ungalimited Arusha, Batuli Hamadi Kisaya amekutana na millardayo.com na Ayo TV na amesimulia mkasa wa kutekwa uliomkuta. Mwalimu huyo anadai kuwa alitekwa na watu wasiojulikana.
Mwalimu
Batuli anasema October 3 mwaka huu wakati akitoka dukani alikutana na
kijana mmoja na aliamriwa kupanda gari walilokuwa nalo, alipokuwa
kwenye gari hilo mmoja wao akamwambia …‘wewe Batuli
ulipoenda kumshtaki mkurugenzi wako uache mara moja na hapo ulipoenda
kulalamika usirudi tena kama unapenda kazi yako, kama unapenda maisha
yako tulia ufundishe na ufunge mdomo unyamaze kimya’
Baaada
ya umbali kidogo Batuli anasema alianza kupiga kelele lakini akawa
amezibwa puani na mdomoni akawa amepoteza fahamu na hakujua
kilichoendelea na alipokuja kushtuka alijikuta Hospitali.
Batuli ameieleza Ayo TV na millardayo.com
kuwa awali kabla ya tukio hilo la yeye kutekwa alipata barua ya kupanda
cheo kuwa mratibu wa Elimu Kata ya Ngarenaro lakini baada ya wiki nne
alipata barua ya kutenguliwa kutoka ofisi ya mkurugenzi. Hata hivyo
alihoji kwa mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro kuhusu kutenguliwa
kwake bila kuambiwa alichokosea.
Kusikiliza Full Stori Bonyeza Play hapa chini
https://youtu.be/fHTGJG_pLpg
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon