Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akijionea kiatu aina ya
Safari buti kinachozalishwa na Kiwanda cha Karanga kilichopo Mkoani
Kilimanjaro wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja kiwandani
katika Mkoa huo. Masauni amesisitiza kiwanda hicho kuzalisha bidhaa bora
zaidi ili kuteka soko kubwa zaidi pamoja na kutekeleza agizo la Rais
Magufuli kuhakikisha majeshi yote nchini yanatumia viatu vinavyozalishwa
na Jeshi hilo. Kulia ni Mkuu wa Kiwanda hicho Mrakibu Msaidizi, Michel
Minja na kushoto ni Ali Jambaraga Fundi Mkuu.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akiangalia kiatu
kilichokuwa tayari kuvaliwa kilichotengenezwa katika kiwanda cha Karanga
kilichopo Gereza Kuu la Karaga mkoani Kilimanjaro. Naibu Waziri huyo
amesisitiza Jeshi hilo kuzidi kutengeneza bidhaa bora zaidi za viatu ili
kuhakikisha wanapata soko kubwa ndani nan je ya nchi., kulia ni
Kamishan Msaidizi Mwandamizi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa
aliye aambatana nae kwenye ziara hiyo.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masaun (aliyevaa koti) akitoa
maelekezo kwa Wakuu wa Gereza la Karanga na kiwanda cha Viatu kilichopo
gerezani hapo. Masauni amelitaka jeshi hilo kuzidi kutoa bidhaa bora ili
kuendelea kuteka soko kubwa ndani nan je ya nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Hamad Masauni, (mwenye tisheti
nyekundu) akielekea kutizama mpaka wa Tarekea wilayani Rombo ili
kujionea changamoto zinazotokana na mipaka hiyo pamoja na kutoa maagizo
kwa viongozi wanaohusika kuimarisha ulinzi wa mpaka huo ili kukabiliana
na upitishaji wa bidhaa za magendo pamoja na wahamiaji haramu ambao
wamekua wakiinia nchini bila vibali. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Jeshi la
Polisi Mkoa wa Kilimaanjaro Kamishna Msaidizi Mwandamizi Wilbrod
Muutafungwa akifatiwa na Kamishna wa Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro,
Mwanguku, na wan ne kutokea kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Rombo Agnes
Hokororo alieambatana na Naibu Waziri huyo kuangalia mipaka hiyo.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni (katikati) akisikiliza
maelezo kutoka kwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kilimajaro
alipotembela mpaka wa Tarakea wilayani Rombo Naibu waziri Masauni
amesema kuwa licha ya changamoto zinazojitokeza katika mipaka yote
miwili ni lazima kuendelea kuimarisha ulinzi kwenye mipaka hiyo na
kudhibiti njia zote zisizo rasmi zinazotumiwa na wahamiaji haramu pamoja
na wafanyabiashara za magendo.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masaun akipewa maelezo na Afisa
Mipaka Holili Michel Amo, juu ya jiwe linaloonyesha mpaka wa Tanzania
na Kenya lililopo katika mpaka wa Holili ambalo limekua likisogezwa na
watu wasiojulikana hivyo kuharibu alama za mipaka. Naibu waziri Masauni
amesema kuwa licha ya changamoto zinazojitokeza katika mipaka yote
miwili ni lazima kuendelea kuimarisha ulinzi kwenye mipaka hiyo na
kudhibiti njia zote zisizo rasmi zinazotumiwa na wahamiaji haramu pamoja
na wafanyabiashara za magendo.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni alipowasili katika
Gereza Kuu la Karanga, Mkoani Kilimanjaro wakati alipotembelea kiwanda
cha viatu kilichopo gerezani haapo ili kujionea uzalishaji wa bidhaa
mbalimbali hasa viatu. Naibu Waziri huyo amelitaka Jeshi hilo kuzidi
kuboresha bidhaa za viatu hivyo ili kujipatia soko kubwa ndanni ya nchi
na kutekeleza agizo la Rais Magufuli kuhakikisha majeshi yote nchini
yanattumia viatu vinavyotengenezwa na Jeshi la Magereza.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akisalimiana na Mkuu wa
Gereza la Karanga, Kamishna Msaaidizi Mkwiche mkoani Kilimanjaro wakati
alipofanya ziara katikaa Kiwanda cha viatu kilichopo katika gereza hilo
ili kujionea uzalishaji wa bidhaa za viatu ambavyo Rais Magufuli
alitaka majeshi yote nchini kutumia viatu vinavyotengenezwa na Jeshi la
Magereza.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akisikiliza maelezo
kuhusu uzalishaji wa viatu katika kIwanda cha Gereza la Karanga kutoka
kwa Fundi Mkuu wa Kiwanda hicho Ali Jambaraga wakati alipofanya ziara
yake kwenda kujionea uzalishaji wa bidhaa mbalimbali lakini pia ametaka
wazidi kuzalisha bidhaa bora zaidi ili kuteka soko la ndani na je ya
nchi ikiwa ni pamoja na kutekeleza agizo la Rais Magufuli kuhakikisha
majeshi yote nchini kutumia viatu vinavyotengenezwa na Jeshi la
Magereza.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masaun aagiza Jeshi la Magereza
kuzidi kuboresha viatu vinavyotengenezwa na kiwanda chao ili kujipatia
soko kubwa ndani ya nchi na nje.
Hayo
aliyasema jana kwa wakuu wa Gereza la karanga na viongozi wa kiwanda
hicho alipofanya ziara yake ya siku moja katika kiwanda cha viatu
kilichopo katika gereza hilo, mkoani Kilimanjaro
Aidha,
Naibu Waziri huyo alisisistiza Jeshi hilo kutekeleza agizo la Rais John
Magufuli kuhakikisha majeshi yote nchini yanatumia viatu
vinavyozalishwa na Jeshi la Magereza, hivyo ni muhimu kuendelea
kuzalisha bidhaa zilizo bora zaidi
Haiingii
akilini maofisa wa majeshi mbalimbali nchini kuagiza viatu nje ya nchi
wakati viwanda vya ndani vinauwezo wa kuzalisha viatu bora zaidi
vinavyodumu kwa muda mrefu kuliko vinavyoagizwa kutoka nje ya nchi,
alisema Masauni.
Masauni
alisema kwamba dhamira ya Serikali ya awamu ya tano ya kuipeleka nchi
katika uchumi wa kati hivyo Jeshi la Magerezaa kupitia kiwanda chake na
miradi mingine mingi halina budi kuendelea kuzidisha kuzalisha viatu
bora vitakavyo kidhi kiwango cha uhitaji na soko ili kukuza uchumi wao
na Serikali kwa ujumla.
Aidha,
katika ziara yake, Naibu Waziri Masauni amesisitiza kuwa ni muhimu
Jeshi hilo kufanya miradi mingi kwa ustadi mkubwa ili kujipatia psa
zitakazosaidia kujiendesha wao kama jeshi na mashirika mengine
yanayounga mkono miradi yao hivyo kutotegemea ruzuku kutoka serikalini.
Waziri
huyo alilipongeza Jeshi hilo kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora
kulinganisha na nyingine zinazoingizwa nchi, hivyo amesisitiza kuzidi
kutengeneza viatu bora zaidi ili kuwa na uwanja mpana wa soko la ndani
nan je ya nchi.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon