WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amepokea zaidi ya sh. milioni 760 zikiwa ni
misaada kwa wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea
mkoani Kagera Septemba 10, mwaka huu.
Amepokea
misaada hiyo kutoka kwa taasisi na wadau mbalimbali likiwemo kundi la
wanawake New Millennium linaloundwa na wake wa viongozi wa Serikali
walio madarakani na waliostaafu.
Makabidhiano
ya michango hiyo, yamefanyika jana jioni (Alhamis, Septemba 29, 2016)
kwa nyakati tofauti kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni
jijini Dar es Salaam pamoja na makazi ya Waziri.
Miongoni
mwa waliokabidhi misaada hiyo ni pamoja Meya wa jiji la Dar es Salaam
Mhe. Isaya Mwita sh. milioni 10, Kampuni ya mabati ya ALFA imekabidhi
mabati yenye thamani ya sh. milioni 50 na kampuni ya Bia Tanzania (TBL)
sh.milioni 100.
Wengine
ni Ofisa Mtendaji Mkuu kampuni ya vinywani baridi ya Pepsi Cola, Bw.
Avinash Jha amekabidhi sh.milioni 50, kampuni ya Round Table pamoja na
wadau wao sh. milioni 57, kampuni ya Wool Worth sh.milioni 20 na
Jumuiya ya Waislam (FIRDAUS) imetoa viti 15 vya walemavu.
Aidha,
kampuni ya Trans Ocean Supplies LTD imetoa sh. milioni 20, Mkuu wa Mkoa
wa Iringa, Mhe. Amina Masenza amekabidhi sh. milioni 18.681,Mbunge wa
Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Shy-Rose Bhanji amekabishi sh. milioni
tano.
Pia
Chama cha Waagizaji Wakubwa wa Mafuta Tanzania kimekabidhi sh. milioni
415.8, kundi la mtanzao wa kijamii la Whatsapp la Papaso, D’jaro Arungu
limekabidhi sh.520,000 na kampuni ya mafuta ya Camel iliyokabidhi mifuko
1,000 ya saruji.
Jumuia
ya Wanataaluma ya Vyuo Vikuu vya Umma Tanzania (ASAs) imekabidhi sh.
milioni 7.5, Umoja wa Wamiliki wa Maduka ya Dawa Muhimu Tanzania
umekabidhi dawa zenye thamani ya sh. milioni tano pamoja na Eric
Shigongo wa Global Publisher amekabidhi mabati 500 yenye thamani ya sh.
milioni 10.
Waziri
Mkuu amewashukuru wadau wote kwa misaada hiyo na kuahidi kuwa Serikali
itahakikisha michango hiyo inafikishwa Kagera kwa walengwa.
“Tunashukuru
sana kwa michango yote. Michango hii ni muhimu na inaonyesha mshikamano
wa dhati uliopo. Michango hii inaonyesha kuguswa na mapenzi ya dhati
kwa waliopatwa na maafa. Amesema.
Akaunti
ya maafa imefunguliwa katika Benki ya CRDB yenye Namba. 015 222 561
7300 kwa jina la KAMATI MAAFA KAGERA – Swiftcode: CORUtztz na namba za
simu za mkononi zinazotumika kupokea michango hiyo ni
0768-196-669(M-Pesa), au 0682-950-009 (Airtel Money) au
0718-069-616(Tigo Pesa).
Tetemeko
hilo lililotokea Jumamosi, Septemba 10, mwaka huu na kusababisha vifo
vya watu 17 na wengine 440 walijeruhiwa kati yao watu 253 walifikishwa
Hospitali ya Mkoa, 153 walilazwa, 113 walitibiwa na kuruhusiwa na
wengine 38 wanaendelea na matibabu ambapo kati yao watu 23 wamefanyiwa
upasuaji mkubwa na wanaendelea vizuri.
Pia
tetemeko hilo limesababisha nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081
zikiwa katika hali hatarishi baada ya kupata nyufa na 9,471 zimepata
uharibifu mdogo huku wananchi 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon