MBUNGE
wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka (CCM), amepata tuzo ya Umoja
wa Mataifa (UN) ikiwa ni mchango wa kuthamini kazi aliyoifanya, huku
akikataa kupokea zawadi ya Dola 100, 000 za Marekani, ambazo ni zaidi ya
Sh milioni 200.
Profesa Tibaijuka alitoa taarifa hiyo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo alisema tuzo hiyo ya Maendeleo Endelevu ilidhaminiwa na mwana Mfalme wa Bahrain, Khalifa bin Salman Al Khalifa.
Alisema,
hatua ya kuzikataa fedha hizo, ni njia ya kukwepa mtego kama uliomkuta
mwaka juzi baada ya kupokea fedha za Escrow Sh bilioni 1.6 kutoka kwa
mfanyabiashara, James Rugemalira.
Tuzo
hiyo ambayo ni heshima kwa Tanzania, alikabidhiwa Septemba 24, mwaka
huu na inajulikana kama ‘His Royal Highness Prince Khalifa bin Salman Al
Khalifa Award for Sustainable Development’.
Profesa Tibaijuka alisema, alikabidhiwa tuzo hiyo kwa kutambua mchango wake katika kuhamasisha maendeleo duniani.
Alisema
tuzo hiyo ya heshima hutolewa kila baada ya miaka miwili na washiriki
wakuu huwa ni wale waliowahi kufanya kazi na Shirika la Umoja wa
Mataifa.
Mwaka huu, Waziri Mkuu wa Bahrain Khalifa bin Salman ndiye aliyemkabidhi tuzo hiyo, alisema.
“Tuzo
hii nimepewa Marekani ikiwa kama sehemu ya kutambua mchangoa wangu
katika kuhamasisha maendeleo na nilikabidhiwa katika Makao Makuu ya UN
na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali duniani.
“Na
huambatana na zawadi ya Dola za Marekani 100,000 (Sh milioni 200).
Sikuzichukua fedha hizi, kama mnavyojua maadili ya nchi yetu unaweza
ukapokea yakaibuka mambo mengine.
“Ingawa
kwenye ule mkutano niliwaambia kuwa sipokei fedha kutokana na hali
halisi … niliwaambia kuwa kama mnavyojua katika mkoa ninaotoka (Kagera)
kuna tetemeko limetokea,” alisema Profesa Tibaijuka.
Alisema
kupokea tuzo hizo si kwa ajili ya mafanikio yake binafsi bali kwa
Watanzania wakiwamo wapiga kura wake wa Muleba Kusini ambao muda wote
wamekuwa wakimtia moyo wa kufanyakazi kwa bidii.
Profesa
Tibaijuka ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, alisema ameuachia Umoja wa Mataifa (UN) na wadhamini wa tuzo
hiyo waamue cha kufanya kuhusu fedha hizo.
Katika
kupokea tuzo hiyo, mbunge huyo alisindikizwa na Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga na
Mbunge wa Viti Maalumu, Anna Lupembe (CCM).
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon