Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Tanzania (TCRA) , jana
December 14 imefanya Ukaguzi wa mwisho, kujiridhisha na kuruhusu Kituo
cha Utangazaji cha Radio5 Arusha kurudisha Matangazo yake hewani ifikapo
December 16 mwaka huu 2016.
Akiongea
na Viongozi na baadhi ya Wafanyakazi wa Radio 5 baada ya kukamilisha
ukaguzi wao, Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA Bw. Fredrick Ntobi alisema
wao kama Mamlaka Waliamua kuja kufanya ukaguzi wao kwa ajili ya
kujiridhisha kurudisha Matangazo ya Kituo hicho hewani December 16
ambapo ndiyo tarehe rasmi ya kuisha kwa adhabu waliyokuwa wametoa kwa
kituo hicho.
Kituo cha Radio 5 kilisimamishwa na TCRA kurusha matangazo yaketoka tarehe 16 September 2016 kwa kukiuka baadhi ya kanuni.
Mamlaka
hiyo ilifanya ukaguzi wa Studio ya Kurusha Matangazo (On air Studio),
Studio ya kuzalisha Vipindi (Production Studio), Chumba cha Habari (News
room), Control Room, ofisi zote za Kituo pamoja na Mnara wa Kurushia
Matangazo ambapo kote wamekuta kila kitu kiko sawa kwa kazi kama Mamlaka
inavyotaka.
Hata hivyo Bw. Fredrick Ntobi akiwa ameongozana na Viongozi wa TCRA kanda ya Kaskazini, aliwakumbusha
Watangazaji na Waandishi kufuata Maadili ya uandishi wa habari ili
kulinda Vituo vyao na Kulinda taaluma zao kwa ajili ya kuendelea
kuhabarisha na kuelimisha Jamii nzima ya Watanzania.
“Mimi
niwasisitize tu kuendelea kufuata maadili ya taaluma yenu ya uandishi
wa habari, kufuata sheria na kanuni za uandishi wa habari ambao
mmesomea, tumieni lugha Sanifu ambayo inakubalika kwa jamii na tasnia
yenu na niwatakie maandalizi mema ya kurudi hewani pamoja na Sikukuu
zinazokuja”. Alimaliza kwa Msisitizo Bw. Fredrick Ntobi.
Hata hivyo kwa upande wa Mkurugenzi wa Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Radio5, Bw. Robert Francis, aliwataka
Wasikilizaji wa Radio5 kukaa mkao wa Kuhabarika, Kupata Burudani na
kuelimika zaidi kupitia Radio5 kwani Wamejipanga vyakutosha kurudi
hewani kwa Kishindo.
“Mimi
niwaombe tu wasikilizaji wetu ambao najua wametumiss sana, wakae tayari
Kuhabarika, kuelimika na kuburudika zaidi sababu mimi na Wafanyakazi
wangu tumejipanga vya kutosha haswa ukizingatia kwamba mwaka mpya ndo
huu unakuja.
"Kingine
niwape pole tu wasikilizaji wetu wote kwa kutotusikia hewani kwa
kipindi cha miezi mitatu, pamoja na Wadau ambao tumekuwa tukishirikiana
kwa pamoja katika mambo mbali mbali niwaambie tu tunarudi rasmi Ijumaa
ya tarehe 16 December 2016”. Alisema Mkurugenzi wa Radio5 Robert Francis.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon