Jeshi
la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limevamia ofisi za mtandao wa
Jamii Forums (JF) na kufanya upekuzi na kuondoka na nyaraka za
usajili wa Jamii Media ikiwemo cheti cha mlipa kodi, cheti cha BRELA,
leseni ya biashara, n.k..
Askari
hao walivamia ofisi hizo jana mchana wakiwa wamefuatana na na
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao huo, Maxence Melo, wakafanya upekuzi na
kuwahoji baadhi ya wafanyakazi.
Baada
ya kufanya upekuzi ndani ya ofisi hiyo walielekea nyumbani kwa
mkurugenzi huyo, kufanya upekuzi kabla ya kumrudisha rumande kwa vile
hakufikishwa mahakamani.
Melo alikamatwa juzi na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi ambako aliwekwa selo.
Anakabiliwa
na mashtaka ya kuzuia upelelezi wa makosa ya mtandao kwa kushindwa
kutoa taarifa binafsi za watumiaji wa mtandao wa Jamii Forums ambazo
polisi walizihitaji.
Taarifa
iliyotolewa jana na mtandao huo iliwataka watumiaji wake kutokuwa na
hofu yoyote na kwamba Jamii Forums haina server Tanzania wala Africa .
"Tunaomba
umma utambue kwamba Jamii Media haina servers wala min-server ofisini
kwake, nchini Tanzania wala Afrika. Pili, tunaomba watumiaji wa
JamiiForums.com wasitiwe wasiwasi juu ya usalama wa taarifa zao.
"Teknolojia
tunayoitumia (encryption) kumsajili mtumiaji wa JamiiForums.com
haituwezeshi kumfahamu mtumiaji yeyote labda yeye akubali kwa hiari yake
kujiweka wazi mtandaoni." Ilieleza taarifa hiyo
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon