Mtoto aanika kisa bosi wake kummwagia mafuta ya moto



MTOTO anayedaiwa kufanyiwa ukatili na mwajiri wake mwenye umri wa miaka 14 (jina limehifadhiwa), na kulazwa katika Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Mbeya kwa matibabu, amesimulia mwanzo mwisho wa mkasa mzima wa tukio hilo.

Akizungumza na wanahabari akiwa amelazwa wodi namba mbili ya hospitali hiyo, mtoto huyo aliyeishia darasa la nne na kuanza kufanya kazi za ndani, alidai kuwa alifanyiwa ukatili huo na mwajiri wake baada ya kuchelewa kupika mboga.

Alidai kuwa akiwa nyumbani kwa bosi wake, Bupe Benjamin, akiandaa mafuta ya kupikia mboga, tajiri wake huyo aliingia ndani na kumhoji kwa nini amechelewa kupika mboga.

"Nilimjibu imetokana na mimi kukabiliwa na majukumu mengi, na bosi wangu aliponyakua mafuta yaliyokuwa motoni na kunimiminia miguuni," alidai.

Alidai kuwa baada ya tukio hilo, bosi wake alimfungia ndani kwa mwezi mmoja na kumuamuru asitoke nje huku akiwa hapatiwi matibabu yoyote.
Previous
Next Post »

COMMUNITY HELP