Watoto
wawili wenye umri wa miaka mitatu na sita wa Kijiji cha Patane Kata ya
Mambamiamba wilayani Same, wameuawa kwa kuchinjwa na panga na baba yao
mzazi Yohana Greson (26) na yeye mwenyewe kujining’iniza kwenye paa la
nyumba.
Akitoa
taarifa kwa vyombo vya habari jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa, alisema tukio hilo lilitokea Desemba
13, mwaka huu majira ya saa tano asubuhi katika Kijiji cha Patane.
Kamanda
alisema baba huyo alifanya tukio hilo la kutisha baada ya mkewe Eva
Tumaini (29) mkazi Kijiji cha Ghona kwenda shambani na kumwacha mumewe
nyumbani akiwa na watoto wawili, Esta Yohana na Tumaini Yohana, ambapo
alichukua panga na kuwachinja na yeye kujinyonga kwa kamba.
Alisema
Polisi inaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na kwamba uchunguzi wa
awali umebaini marehemu huyo alikuwa na tatizo la kifafa.
Alisema
miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Same
kwa ajili ya uchunguzi zaidi na kwamba marehemu hakuacha ujumbe wowote
na uchunguzi ukikamilika ndugu za marehemu watakabidhiwa miili hiyo kwa
ajili mazishi.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon