Shirika
la Nyumba la Taifa (NHC), limewasilisha ripoti ya wadaiwa sugu wa
shirika hilo, zikiwamo wizara, taasisi za Serikali na watu binafsi kwa
Rais Dk. John Magufuli, huku wizara mbili zikiwa na deni kubwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mikoa na
Utawala wa NHC, Raymond Mndolwa, alisema uamuzi huo umekuja baada ya
Rais Magufuli kuwataka kukusanya madeni hayo na kuwasilisha taarifa hiyo
ofisini kwake ili aweze kuipitia.
Mndolwa
alisema NHC ilitoa notisi ya siku 90 ambayo ilianza Septemba, mwaka
huu, huku wadaiwa hao wakitakiwa kulipa madeni ndani ya muda
uliopangwa.
Alisema
kuwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto na
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo bado zinadaiwa kiasi
kikubwa cha fedha, licha ya kuwapo kwa mazungumzo ya kulipa madeni yao.
“Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto inadaiwa Sh
bilioni 1.4, huku wakilipa Sh milioni 300, wakati Wizara ya Habari,
inadaiwa Sh bilioni 1.14, lakini imelipa Sh milioni 700,” alisema Mndolwa.
Mndolwa
alisema shirika hilo hadi sasa limekusanya Sh bilioni 5.9 kati ya Sh
bilioni 9.3 ambalo ni deni la Serikali kupitia wizara na taasisi
mbalimbali, huku Sh bilioni 2.5 zikikusanywa kutoka kwa wadaiwa binafsi
ambao awali walikuwa wanadaiwa Sh bilioni 4.
Alisema
lengo la shirika hilo ni kuhakikisha madeni yanalipwa ili fedha hizo
ziweze kutumika kwenye shughuli nyingine za maendeleo, ikiwamo ujenzi wa
nyumba za kisasa 300 mkoani Dodoma.
Alizitaja
wizara zinazodaiwa ni Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Fedha na
Uchumi, Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Kilimo, Mifugo na
Uvuvi na iliyokuwa Wizara ya Ujenzi.
Wadaiwa wengine ni Ofisi ya Waziri Mkuu, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon