Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,
amempongeza Balozi Prof. Joram Mukama Biswaro kwa kuteuliwa kuwa
Mwakilishi Maalum wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika na Mkuu
wa Ofisi ya Umoja huo Sudan Kusini.
Balozi
Prof. Joram Mukama Biswaro ameteuliwa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya
Umoja wa Afrika (AU) Dkt. Nkosazana Dlamini-Zuma na anachukua nafasi
iliyoachwa wazi na Brigedia Jenerali Sara Thomas Rwambali ambaye
amemaliza muda wake.
Katika
pongezi hizo Rais Magufuli amesema Tanzania imepokea uteuzi huo kwa
heshima kubwa na ipo tayari kutoa ushirikiano wowote utakaohitaji kwa
Balozi Joram Mukama Biswaro katika utekelezaji wa majukumu yake.
“Natambua
kazi kubwa iliyopo mbele yako katika nafasi hiyo muhimu ndani ya Umoja
wa Afrika (AU), hata hivyo kwa kutambua uwezo wako, uzoefu wako na
uchapakazi wako naamini kuwa utatekeleza majukumu yako kwa viwango vya
hali ya juu na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Dkt. Nkosazana
Dlamini-Zuma hatajutia uamuzi wake wa kukuteua katika nafasi hiyo” amesema Rais Magufuli.
Dkt.
Magufuli amemtakia heri Balozi Prof. Joram Mukama Biswaro katika
majukumu hayo mapya, na amemshukuru na kumpongeza Brigedia Jenerali Sara
Thomas Rwambali aliyemaliza muda wake kwa uwakilishi mzuri katika
kipindi chake.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon