Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameahidi
kukutana na wafanyabiashara wa soko la Sabasaba mkoani Dodoma ili
kuzungumzia namna ya kulikarabati na kulifanya liwe la kisasa.
Amesema miongoni mwa mambo watakayoyajadili katika kikao hicho ambacho hakutaja siku ni pamoja na kuboresha mazingira ya kufanyia biashara hasa kwa wanaouza bidhaa nje ya maduka.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo Jumatano, Oktoba 5, 2016wakati
alipotembelea maduka hayo yaliyoko katika barabara ya One Way inayopita
katikati ya barabara ya sita hadi ya 11 pamoja na soko la Sabasaba akiwa
kwenye ziara ya kukagua maeneo ya kutolea huduma za jamii mjini Dodoma.
Alisema Serikali tayari imeshahamia Dodoma hivyo wafanyabiashara
wanatakiwa kutumia fursa hiyo kwa kuboresha biashara zao ili waweze
kumudu ushindani wa soko.
“Wafanyabiashara lazima mboreshe biashara zenu, muongeze usafi zaidi
na ikiwezekana muimarishe majengo yenu yawe ya kisasa zaidi kwani
haiwezekani maduka ya Makao Makuu ya Nchi yawe katika hali hii,”
alisema.
Pia Waziri Mkuu aliwataka wafanyabiashara hao wasiogope kwenda kukopa
katika taasisi mbalimbali za kifedha kwa lengo la kujiongeza mitaji na
kupanua biashara.
Alisema tayari alishatoa maagizo kwa wamiliki wa benki kuhakikisha
wanawawezesha wajasiriamali wadogo kwa kuwapa mikopo, hivyo aliwataka
wasiogope na badala yake wachangamkie fursa hiyo.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon