ctober 11 2016 Mabalozi wa Jamhuri ya Muuungano ya Tanzania walioko nchi za nje walitembelea hospitali ya Kisasa kujionea Ujenzi wa kampasi ya chuo na hospitali ya taaluma na tiba ya chuo kikuu cha afya na sayanzi shirikishi, Muhimbili.
Hospitali
hiyo ipo Mloganzila Dar es salaam, kitu cha kufahamu ni kuwa itakuwa na
ghorofa tisa, vyumba vya upasuaji kumi, mashine za kufanyia uchunguzi za
kisasa, wodi za kulaza wagonjwa karibu flow tano za kisasa na wodi
zingine. Makamu mkuu wa chuo Prof. Ephata Kaaya kaelezea mambo muhimu
ambayo kampasi ya chuo na hospitali ya Taaluma na Tiba, ya chuo kikuu
cha afya na sayanzi shirikishi, Muhimbili itakuwa nayo………..
>>>
‘Kampasi hii ikikamilika, chuo kitaweza kuongeza udahili wa wanafuzni
kutoka 4,000 waliopo sasa hadi 15,000, kufanya tafiti nyingi zenye ubora
na zinazolenga matatizo ya wananchi wetu na kutoa huduma za afya kwa
kiwango cha juu kwa wananchi’
>>>’Hospitali
hii ni ya kisasa na itatoa huduma za afya za hali ya juu, mafunzo bora
kwa wanafunzi wa fani ya afya, uchunguzi wa magonjwa na tafiti zenye
ubora katika fani za afya hapa nchini. Itakapoanza kutumika, hospitali
hii itapunguza kwa kiasi idadi ya wagonjwa na gharama zinazotumika
kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu’;- Prof. Ephata Kaaya
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon