Na Is-haka Omar, Zanzibar.
WAJUMBE
wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wameshauriwa kuondosha mfumo wa
Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) katika Katiba ya Zanzibar ya Mwaka
mwaka 1984.
Ushauri
huo umetolewa na Katibu wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa kimataifa wa
Kamati Maalum ya NEC, CCM Zanzibar, Hamad Yussuf Masauni katika
Majumuisho ya ziara yake ya kuimarisha uhai wa Chama huko katika Ukumbi
wa Amani Mkoa wa Mjini, Unguja.
Alisema
huu ndio wakati mwafaka wa kuondosha mfumo huo kwani hauna tija katika
maendeleo ya nchi badala yake ukiachwa itakuwa ni fursa kwa wapinzani
kurudi tena katika serikali baada ya kufanyika Uchaguzi Mkuu ujao wa
mwaka 2020.
Alieleza
kwamba nia ya CCM kukubali kuingia katika mfumo wa Serikali ya Umoja wa
kitaifa (SUK) ni kushirikiana na vyama vya upinzani katika mipango ya
maendeleo ya nchi pamoja na kumaliza siasa za chuki, hali ambayo CUF
haikutaka kubadilika hivyo hakuna haja ya kubakisha mfumo huo katika
Katiba ya Zanzibar.
Masauni
aliwasihi Wawakilishi wa CCM kuhakikisha wanalinda kwa vitendo maslahi
ya Chama kwa kuandaa taratibu zote za kisheria kwa kufuta kipengele
ndani ya Katiba kinachoeleza uwepo wa mfumo huo.
Alisema
hatua ya mwisho itakuwa kurudi kwa wananchi kupiga kura ya maoni ya
kukubali ama kukataa kuendelea na SUK, jambo ambalo kwa sasa ni rahisi
kwani wananchi wengi hasa wafuasi wa CCM hawataki kuendelea na serikali
hiyo.
“
Huu ni wakati mwafaka wa kuifuta CUF katika siasa za Zanzibar kwani
hatuwezi kuendelea kuwa na ushirikiano na Chama kinachojali maslahi
binafsi pamoja sera za utengano badala ya kuwaunganisha wananchi.
Hakuna
haja ya kuendelea na SUK kwani katika miaka mitano ya mfumo huo wenzetu
walionyesha udhaifu mkubwa na kupelekea nchi kuanza kuyumba kwani hata
viongozi wao wa majimbo hawakufanya chochote kwa wananchi na mzigo wote
waliwasukumia viongozi wa CCM.”, alisema Masauni na kuongeza kuwa
serikali iliyopo sasa inaendelea kuwatumikia wananchi wote bila ya
ubaguzi.
Aliwapongeza
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa juhudi zao za kufanya mabadiliko
ya baadhi ya sheria ndani ya Katiba ya Zanzibar zilizokuwa zikiwajengea
ngome ya kujiamini chama cha CUF katika Baraza hilo.
Akizungumzia
Uchaguzi wa ndani ya CCM unaotarajiwa kufanyika mwaka 2017, Masauni
alikemea tabia na vitendo vya kuendekeza siasa za makundi ndani ya CCM
kwani hali hiyo aliitaja kuwa inasababisha kupatikana kwa viongozi
wasiokuwa waadilifu ndani ya chama hicho.
Alisema
baadhi ya viongozi wa CCM wanatakiwa kuwakataa watu watakaoingia ndani
ya Chama hicho kuwania nafasi za uongozi kupitia nguvu za fedha na
umaarufu kwani watu hao ndiyo chanzo cha kujengeka makundi yasiyokuwa na
lazima ndani ya chama chetu.
“
Sote tunakumbuka athari mbaya ya makundi iliyojitokeza katika chaguzi
zilizopita na kuendelea kutusumbua mpaka sasa kwani kuna baadhi ya
wanachama waliweka mbele maslahi ya watu binafsi badala ya CCM.”,
alifafanua Masauni.
Masauni
ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, alieleza kwamba
serikali haitovumilia kuona vitendo vya uhalifu vinaendelea katika
maeneo mbali mbali ya Zanzibar, na wanaofanya vitendo hivyo waache kabla
hawajachukuliwa hatua za kisheria.
Aliwataka
wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama
ili kupunguza kesi za uhalifu unaotokea katika maeneo mbali mbali nchini
kwani kuna baadhi ya wananchi wanakataa kutoa ushahidi kwa watu
wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu.
Mapema
akizungumza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini, Bora afya Silima Juma
aliwapongeza baadhi ya viongozi wa Majimbo wanaotekeleza vizuri Ilani ya
CCM ya mwaka 2015/2020 kwa wananchi.
Alisema
tokea kumalizika kwa Uchaguzi wa Marudio hali ya kisiasa ndani ya Mkoa
huo imeimarika kwani kila mwanachama na wananchi kwa ujumla wamekuwa
wakifanya kazi za kujitafutia kipato bila ya usumbufu.
Nao
wanachama wa Chama hicho, waliahidi kutoa ushirikiano kwa mambo mbali
mbali yatakayoiwezesha CCM kurudi madarakani katika uchaguzi Mkuu ujao.
Walipongeza
juhudi zinazofanywa na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein na Rais
wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa kutekeleza
ahadi mbali mbali walizoahidi wananchi katika kampeni za Uchaguzi
uliopita.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon