
Bondia
maarufu wa ngumi za kulipwa nchini, Thomas Mashali amefariki dunia
usiku wa kuamkia leo October 31 2016 maeneo ya Kimara DSM, Taarifa
zinadai kuwa alishambuliwa na wananchi baada ya madai ya kuitiwa mwizi.
Taarifa
kutoka kwa Promota wake, Siraji Kaike amesema watu aliokuwa anagombana
nao walimwitia mwizi na wakawa wamemshambulia na baadaye wakawa
wamemtupa na bodaboda waliokuwa wanamjua Thomas Mashali walimuokota na
kumpeleka hospitali ambapo baadaye zilitolewa taarifa kuwa amefariki.

Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon