WEMA Sepetu Akunwa na Wimbo wa Diamond 'Salome' Ajirekodi Akiimba, Diamond Asema Haya

Malkia wa filamu Wema Sepetu amekunwa na wimbo mpya wa Diamond Platnumz ‘Salome’ na kuamua kujirekodi video huku akiimba wimbo huo.

Diamond alipost video instagram inayomwonyesha mwigizaji huyo akiimba wimbo ‘Salome’ huku akiandika ujumbe wa kuonyesha kufurahishwa na kitendo hicho.

“Hivi huku patakuwa ni kupatwa kwa nini?. Tisha sana ‘Salome’ wake Idris Sultan full Video link in my BIO and @rayvanny Bio,” aliandika Diamond kupitia instagram.

Hatua hiyo huwenda ikafungua njia zaidi kwa wawili hao kuaidia katika mambo yao.
Previous
Next Post »

COMMUNITY HELP