UTAFITI: Twaweza wametoa ripoti hii kuhusu suala la Udikteta nchini














Leo September 29, 2016 Taasisi ya Twaweza wamefanya uzinduzi wa ripoti ya utafiti mpya jijini Dar es salaam. Utafiti huo unaeleza kuwa Watanzania wengi hawaoni kama nchi inaendeshwa kidikteta baada ya mtu mmoja kati ya 10 waliohojiwa kueleza nchi inaongozwa kwa mfumo huo. 
ctdged0xgaaoqjc
Matokeo ya utafiti huo uliofanywa kwa njia ya simu kati ya Septemba 24-29 mwaka yanasema kuwa watu sita kati ya 10 sawa na asilimia 58 walipinga kuwa nchi inaongozwa kidikteta huku asilimia 31 wakieleza kutokuwa na uhakika. Katika utafiti huo unaoitwa “Demokrasia, udikteta na maandamano: wananchi wanasemaje”, mwananchi mmoja kati ya watatu alitafsiri udikteta kuwa ni kitendo cha Serikali kutumia nguvu wakati wa kuitawala nchi.
ctdh1xpw8aabgwq
Licha ya wananchi wengi kueleza hawaoni nchi ikiongozwa kidikteta, ripoti hiyo iliyohoji watu 1,602 wa Tanzania Bara inaeleza kuwa wananchi saba kati ya 10 wanaunga mkono demokrasia kama mfumo bora wa Serikali, mtazamo ambao unaoshabihiana na wafuasi wa vyama mbalimbali nchini.
Pamoja na kuhoji masuala mbalimbali namna nchi inavyoendeshwa, Twaweza walihoji watu pia ufuasi wao kwa vyama vya siasa ambapo asilimia 66 walieleza kuwa karibu na CCM huku asilimia 19 wakiwa karibu na upinzani hususan Chadema. Watu wawili kati ya 10 (asilimia 15) walisema hawana ukaribu na chama chochote.



Previous
Next Post »

COMMUNITY HELP