
Masaa kadhaa baada ya mtu mmoja ambaye ni raia wa Uganda kupigwa risasi na kuuawa na polisi mjini California siku ya Jumatano, Serikali ya nchi hiyo imetoa agizo kwa Ubalozi wake jijini Washington DC nchini Marekani, kuchukuza na kutoa maelezo ya kina mazingira yaliyosababisha kifo cha raia wake Alfred Olango.
Msemaji wa
Wizara ya Mambo ya nje ya Uganda Margaret Kafeero ameliambia Gazeti la
kila siku nchini Uganda la Daily Moniter kuwa, Serikali imemtaka Balozi
wa Uganda kufanya uchunguzi wake, ili kubaini kilichosababisha Olango
kupigwa risasi.
>>>>Tumemwagiza
Balozi wetu mjini Washington DC kutafuta ukweli wa jambo hili kwa
sababu kile tunachokifahamu tu ni kuwa, raia wetu amepigwa risasi na
kuuawa:- Amesema Waziri Kafeero.
Polisi
nchini Marekani wamekiri kuwa, raia huyo wa Uganda mwenye umri wa miaka
30 alipigwa risasi baada ya kuonekana alitoa kitu mfukoni katika
makabiliano na maafisa wa polisi, hata hivyo, polisi wamesema mtu huyo hakuwa amebeba silaha wakati wa tukio hilo
Baada ya tukio hilo, Wamarekani weusi na raia wengine weusi waljitokeza na kuanza kuandamana kulaani mauaji hayo na imebainika
kuwa, Olango alikuwa ni mkimbizi kutoka nchini Uganda lakini pia
alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya akili, suala ambalo pia huenda
lilichangia makabiliano yake na polisi.
Polisi
wamesisitiza kuwa, walimwagiza atoe mikono mifukoni mwa suruali yake
lakini akatoa kitu ambacho kimebainika kuwa sigara ya kieletroniki, Marekani imeendelea kushuhudia vifo vya Wamarekani na wahamiaji haramu mikononi mwa polisi wazungu.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon